Mafunzo ya awali ya uchunguzi kwa waajiriwa wapya 553 wa TAKUKURU yamehitimishwa leo Septemba 19, 2022.

Mafunzo haya yaliyokuwa yakifanyika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi yamehitimishwa rasmi na Mhe. Deogratius Ndejembi – Naibu Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.