“…Ustawi wa maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini hauwezi kufanikiwa bila kuhakikisha tunadhibiti uwepo wa mianya au vitendo vya rushwa katika sekta ya michezo…” CP. Salum Rashid Hamduni, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amesema hayo wakati akifungua kikao kazi kilichojadili taarifa ya uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa fedha za maendeleo ya mpira wa miguu na kuweka mikakati ya kudhibiti mianya iliyobainishwa. Kikao hiki kimefanyika Hoteli ya Rafiki, Dodoma na washiriki walitoka TAKUKURU, TFF, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo; Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Baraza la Michezo Tanzania pamoja na TRA, Septemba 15, 2022.