CP. Salum Hamduni – Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Viongozi wa nchi wanachama wa utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Rushwa (Intersessional Meeting of the Conference of State Parties to the UNCAC on the achievements of the political declaration adopted by the special session of the General Assembly –UNGASS).
Mkutano huu wa siku nne ulianza Septemba 5 hadi tarehe 8, 2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa jijini Vienna, Austria ambapo ajenda kuu ni kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Rushwa. Kupitia mkutano huu, kila nchi mwanachama ikiwemo Tanzania ilitakiwa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji kwa maeneo yafuatayo: –
- Preventive Measures
- Criminalization and Law information
- International Cooperation
- Asset Recovery
- Technical Assistance and information exchange
- Anti – Corruption as an enabler of 2030 Sustainable Development
- Advancing way forward of anti-corruption agenda
Katika mkutano huu, Mkurugenzi Mkuu aliongozana na Wataalam wa utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UNCAC Governmental Experts) kutoka TAKUKURU, FIU pamoja na Ofisi ya Rais Ikulu – Idara ya Uratibu wa Utawala Bora na Maboresho (GGCR).