Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye, ameongoza ujumbe wa Maafisa Waandamizi wa TAKUKURU wanaoshiriki Mkutano wa 44 wa ‘The Eastern and Southern Africa Anti-Money Laundering Group (ESAAMLG), unaofanyika nchini Zambia. Mkutano huu unaohusu masuala ya Udhibiti wa Fedha Haramu Kusini mwa Jangwa la Sahara unahudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Mkurugenzi wa Mashtaka pamoja na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya. Aidha, Mkutano huu utafuatiwa na Mkutano wa 22 wa Baraza la Mawaziri wa ESAAMLG na Kikao cha 5 cha Mazungumzo kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi lengo likiwa ni kujadili masuala ya udhibiti wa fedha haramu. Mkutano huu umeanza Agosti 28, 2022 na utahitimishwa Septemba 3, 2022. Washiriki wengine kutoka TAKUKURU ni Bw. Donassian Kessy ambaye ni Focol Person wa ESAAMLG na Bi. Lilian William ambaye ni Rais wa ARINEA.