Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama, amehitimisha Mafunzo ya Kati ya Uchunguzi kwa maafisa 99 wa TAKUKURU waliohitimu mafunzo hayo Agosti 19, 2022. Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo iliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha mkoani Pwani na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, Waziri Mhagama ameilekeza TAKUKURU kuhakikisha inakuwa na mikakati ya kujenga mazingira ya KUZUIA RUSHWA na kuifanya kuwa shirikishi na karibu zaidi na wananchi. Amesema kwa kufanya hivyo, TAKUKURU itaweza kupokea taarifa nyingi zaidi za uwepo wa viashiria vya rushwa kabla haijatokea.