Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye, amefanya ziara ya kukagua hatua za ujenzi wa ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Ziara hiyo imefanyika Agosti 15, 2022 akiwa ameongozana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa DODOMA Bw. Sosthenes Kibwengo (wa kwanza kushoto picha ya juu). Wengine ni Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kongwa Bw. Cosmas Shauri ( wa pili kulia) na Afisa wa Kurugenzi ya Usimamizi wa Miliki TAKUKURU Bw Joseph Kobelo (wa kwanza kulia). Kwa mujibu wa maelezo ya kitaalamu yaliyotolewa, ujenzi wa jengo hili umefikia kiwango cha asilimia 95.