Menejimenti za Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, wamefanya Kikao Kazi cha pamoja jijini Dodoma Agosti 11, 2022.
Kikao Kazi hicho kimefanyika kwa lengo la kujadili mafanikio, changamoto pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha utendaji kazi katika usimamizi wa MNYORORO WA HAKI JINAI nchini. Kikao hiki ambacho ni mwendelezo wa kikao kama hiki kilichofanyika Julai 2021 na kitaendelea tena Agosti 12, 2022 ambapo kitashirikisha Wakuu wa TAKUKURU Mikoa, Wakuu wa Upelelezi Mikoa pamoja na Wakuu wa Mashtaka Mikoa.