MKUTANO WA 24 WA KAMATI YA MAWAZIRI – SADC

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP. Salum Rashid Hamduni, amehudhuria mkutano wa 24 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (MCO) wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC. Mkutano huu umefanyika kuanzia Julai 16 hadi 19, 2022, jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri umeongozwa na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ameambatana na Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax (Mb.), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Ajenda zilizojadiliwa katika mkutano huu zilihusu Siasa, Ulinzi na Usalama ikiwemo utekelezaji wa Itifaki ya SADC ya Kupambana na Rushwa.

Taarifa kwa Umma