Pichani juu, walioketi ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa (pili kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Saimon Maembe (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa kikao kazi baina ya taasisi hizo, Julai 8, 2022.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), zimekusudia kuwa na mashirikiano ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Serikali.
Katika kufanikisha hilo, taasisi hizo zimekutana katika kikao kazi cha siku mbili tarehe 8 na 9 Julai, 2022, katika Ukumbi wa Mikutano Nashera, mkoani Morogoro, kujadili maeneo ya muhimu ya ushirikiano na changamoto zinazojitokeza wakati wa kutekeleza majukumu.