Juni 29.06.2022, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea Ujenzi wa Uzio wa Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chamwino mkoani DODOMA. Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi Mkuu pia amefanya Kikao Kazi na kuzungumza na watumishi wa ofisi hiyo. Pamoja na Mkurugenzi Mkuu, katika ziara hiyo alikuwepo Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki TAKUKURU Mha. Dkt. Emmanuel Kiyabo (aliyeketi katikati kulia picha ya juu); Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo – aliyeketi kulia kwa Mha. Dkt. Kiyabo pamoja na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Chamwino Bi. Sipha aliyeketi kushoto kwa Mha. Dkt. Kiyabo.