TAKUKURU imeitisha Warsha ya Wadau kujadili na kutoa maoni kuhusu MPANGO MKAKATI WA TAKUKURU wa Mwaka 2022 – 2026. Warsha hii inayofanyika hoteli ya Rafiki jijini DODOMA, imejumuisha Wadau Idara za Serikali. Pichani juu, aliyeketi katikati ni Bi. Sabina Seja, Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa TAKUKURU, kushoto kwake ni Dkt. Titus Mwageni – Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo cha Mipango, DODOMA ambaye pia ndiye Mshauri Mwelekezi katika uandaaji wa Mpango Mkakati huu, pamoja na Bi. Joyce Shirima – Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini TAKUKURU aliyeketi kulia kwa Bi Sabina.