“Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya mtakayoyapata yatakwenda kuleta mabadiliko chanya katika utendaji kazi wenu na kwa watu mtakao wahudumia”. Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye Juni 27, 2022, wakati akifungua mafunzo ya “Intermediate Investigation Course” yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwl. Julius Nyerere – Kibaha, Pwani. Pichani juu waliosimama ni baadhi ya watumishi wa TAKUKURU wanaoshiriki mafunzo hayo na waliokaa ni Viongozi wa TAKUKURU akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu aliyeketi katikati. Wengine ni Mkuu wa Shule ya Uongozi Prof. Marcelino Chijoriga (wa pili kulia) na kushoto kwake ni Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Bw. Christopher Myava. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu TAKUKURU Bw. Ayoub Akida na kulia kwake ni Mratibu wa mafunzo kutoka TAKUKURU Bw. Benjamin Kapera.