KIKAO KAZI

Pichani, aliyesimama mbele wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Frida Wikesi, akiwa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Edward Mwenda ( kushoto kwake), Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa Bi Grace Malagila (kulia kwake) pamoja na Afisa Uchunguzi (Mwanasheria), Furahini Kibanga, wa kwanza kulia. Wengine ni Watumishi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, waliopiga picha ya pamoja mara baada ya kuelimishwa kuhusu Maadili, Uzalendo, Rushwa, Madhara ya Rushwa na Namna wanavyotakiwa kushiriki katika mapambano dhidi ya Rushwa. Elimu hiyo imetolewa Juni 27, 2022.