Juni 22, 2022, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 5 wa Viongozi wa Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika – Africa Association of Anti Corruption Authorities- AAACA, pamoja na mambo mengine wamefanya uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Tendaji (Executive Committee) ya AAACA. Kupitia uchaguzi huo, Tanzania kupitia TAKUKURU imefanikiwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Mjumbe wa Kamati hiyo. Pichani ni viongozi wawakilishi wa Kamati hiyo akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Radhid Hamduni, wa pili kutoka kushoto. Wajumbe wengine ni kutoka Congo Brazavile, Algeria, Zimbabwe na Siera Leone. Mkutano huu unafanyika Bujumbura – Burundi.
Pia wamemchagua Rais kutoka Misri, Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka Mali na Makamu wa Pili wa Rais kutoka Cameroon.