Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka Maafisa Waandamizi wa TAKUKURU kufanya jitihada kubwa za kuzuia mianya ya rushwa kabla haijatokea. Haya yalisemwa wakati wa kuhitimisha Mafunzo ya ‘Senior Investigation Course’ tarehe 17 Juni, 2022. Mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa TAKUKURU yalifanyika kuanzia Juni 6 – 17, 2022 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyoko Kibaha mkoani Pwani.