Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, anahudhuria Mkutano Mkuu wa 5 wa Viongozi wa Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika (The African Association of Anti- Corruption Authorities – AAACA).
Mkutano huu unaofanyika Bujumbura nchini Burundi, unawakutanisha Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi wanachama wa AAACA chini ya Kauli Mbiu isemayo “Protecting Africa’s Wealth: Combating Corruption and Illicit Financial Flows.’ Pamoja na nchi wanachama, wadau wengine wafuatao wanahudhuria mkutano huu wenye lengo la kujadili utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
