RUVUMA, OKT – DES 2021

MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10 YAKAGULIWA NA TAKUKURU RUVUMA.

Ndugu wanahabari.

Leo Januari 25, 2022 tumekutana tena katika ofisi yetu ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma ili kupitia ninyi tuweze kuuhabarisha umma kuhusu utendaji kazi wa ofisi yetu kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi wa Oktoba 2021 hadi Disemba 2021.

Kwa mujibu kifungu cha 7 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, TAKUKURU inayo majukumu makuu matatu ambayo ni; Kuelimisha Jamii juu ya rushwa na madhara yake; Kufanya chambuzi za mifumo kwenye taasisi za umma na sekta binafsi pamoja na kufanya uchunguzi na kufikisha watuhumiwa mahakamani kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) baada ya chunguzi hizo kukamilika.Katika kipindi hiki cha miezi mitatu TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma tulitekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia sheria hii.

Ndugu wanahabari.

UCHUNGUZI

Katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2021, TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, ilipokea jumla ya taarifa mpya 72 za malalamiko mbalimbali. Kati ya taarifa hizo, taarifa 39 zilihusu rushwa na uchunguzi wake bado unaendelea. Aidha taarifa 33 hazikuhusu rushwa hivyo walalamikaji walishauriwa na kuelekezwa kupata msaada kwenye taasisi husika.

Taarifa hizo 72 za malalamiko zilizopokelewa zilihusu maeneo yafuatayo:  Serikali za Mitaa 17, fedha 11, ardhi 9, afya 6, na elimu 6. Nyingine ni maji 3, malalamiko binafsi 3, polisi 3, maliasili 2, ujenzi 2, vyama vya ushirika 2, ustawi wa jamii 1, mahakama 1, kilimo 1, biashara 1, ulinzi 1, TASAF 1, Mifugo 1 na Bima 1.

MASHTAKA

Katika kipindi hiki, kesi nne (4) ziliamuliwa mahakamani, ambapo kati ya hizo TAKUKURU imeshinda kesi 3 na kushindwa kesi 1.

Ndugu wanahabari.

UZUIAJI RUSHWA

Katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2021, TAKUKURU mkoa wa Ruvuma imefanya chambuzi za mfumo saba (7) kuhusu viashiria vya rushwa ya ngono katika sekta ya elimu katika Halmashauri saba za mkoa wa Ruvuma. Aidha tulifuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko-19 yenye thamani ya jumla ya shilingi Bilioni kumi na milioni mia tatu naishirini, (10,320,000,000/=).

Miradi hii ni ya ujenzi wa vyumba 448 vya madarasa katika shule za sekondari wenye thamani ya shilingi bilioni nane namilioni mia tisa sitini (8,960,000,000/=), ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa katika vituo shikizi kwa shule 19 za msingi kwa thamani ya shilingi bilioni moja na milioni arobaini (1,040,000,000/=) pamoja na ujenzi wa mabweni 4 katika shule za msingizenye wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa thamani ya shilingi milioni mia tatu na ishirini (320,000,000/=).

Lengo la ufuatiliaji huu likiwa ni kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa wakati ikiwa na ubora unaolingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi wa miradi hiyo ambayo yangeweza kusababisha mianya ya rushwa, yameweza kufanyiwa kazi kwa kufanya vikao na wadau wa miradi husika pamoja na kutoa elimu kwa lengo la kuondoa mianya ya rushwa iliyopo na kuimarisha usimamizi wa miradi kwa kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni za manunuzi ya umma ili kupata miradi bora yenye kukidhi thamani ya fedha (Value for money).

Ndugu wanahabari.

ELIMU KWA UMMA

Katika kipindi hiki, TAKUKURU mkoa wa Ruvuma ilielimisha makundi mbalimbali ya jamii lengo likiwa ni kuendelea kuwajengea uelewa wa madhara ya rushwa, ili waweze kushiriki katika mapambano haya. Kupitia uelimishaji huo tumeweza kuwafikia wananchi kwa njia ya semina 44 ,pia tuliimarisha  klabu za wapinga rushwa 38 za shule za msingi na sekondari,tuliandaa  Makala 5, tulirusha kipindi kimoja (1) cha redio kupitia Jogoo Fm.

TAKUKURU INAYOTEMBEA

TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma iliendelea na zoezi la kutembelea wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kusikiliza kero za rushwa. Katika kipindi cha miezi mitatu tumefanikiwa kufanya mikutano 18 kupitia utaratibu wa TAKUKURU INAYOTEMBEA na kupokea kero mbalimbali za rushwa na makosa mengine. Taarifa nyingi tulizozipokea hazikuhusiana na rushwa na tuliwasaidia waathirika kupata majibu kutoka kwenye mamlaka walizokuwa wanazilalamikia.

Ndugu wanahabari.

USHIRIKIANO NA WADAU

TAKUKURU Mkoa wa RUVUMA tunathamini ushirikiano tunaoupata kutoka kwa wananchi kwani sasa hivi wananchi wengi wamekuwa wakitupigia simu namba 113 na ile ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa na kueleza matatizo yanayowasibu na wengine wamekuwa wakipiga simu hata kuomba ushauri wa kisheria pale ambapo hata wao wanaelewa kuwa matatizo yanayowakabili siyo ya Rushwa.

Vile vile tuna ushirikiano mzuri na waandishi wa habari na mmekuwa hamtuangushi pindi tunapohitaji huduma yenu. Aidha tupo katika utekelezaji wa mpango wa ushirikiano kati ya TAKUKURU na Skauti ambapo vijana wa Skauti wa Mkoa wa Ruvuma watasaidia katika kuelimisha wanafunzi na vijana rika juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Ndugu wanahabari.

MATARAJIO YETU KWA KIPINDI CHA MIEZI MITATU IJAYO.

Katika kipindi cha miezi mitatu ijayo kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2022 tumejipanga kufanya mambo yafuatayo: –

  1. Kuendelea kuelimisha wananchi juu ya rushwa na madhara yake katika usimamizi wa miradi ya maendeleo lengo ni kuwawezesha wananchi kupata uelewa na kuweza kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa karibu na weledi wa hali ya juu.
  2. Tutaendelea kufanya kazi za uzuiaji rushwa kwa lengo la kubaini mianya ya rushwa katika maeneo mbalimbali zikiwemo taasisi za Umma na Binafsi na kushauri namna bora ya kuiziba mianya hiyo.
  • Tutaendelea kufanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa na kuwachukul