Ndugu WanaHabari;
Habari za asubuhi;
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia sote fursa ya kukutana na kupashana habari kuhusu mambo ambayo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Njombe imeyatekeleza katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba, 2021. Katika kipindi husika, TAKUKURU Mkoa wa Njombe imetekeleza majukumu ya Uelimishaji, Uzuiaji vitendo vya Rushwa na Uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2019.
Ndugu WanaHabari;
UELIMISHAJI
TAKUKURU Mkoa wa Njombe kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba, 2021 tumefanya uelimishaji kwa makundi mbalimbali ambayo ni pamoja na wananchi kupitia mikutano ya hadhara ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa TAKUKURU INAYOTEMBEA,wanafunzi katika baadhi ya shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mkoa, Watumishi wa mamlaka ya Maji Mjini na Vijijini (RUWASA) Njombe, Wasimamizi wa mitihani ya Taifa ya kidato cha pili na kidato cha nne, Jeshi la Akiba pamoja na watumishi mbalimbali wa Sekta Binafsi.Uelimishaji huo umefanyika kwa njia ya Semina, Mikutano ya hadhara na Maonesho. Hivyo basi katika kipindi CHA MWEZI Oktoba hadi Disemba, 2021 tumefanya Semina 25, Mikutano ya Hadhara 11, Maonesho 02 na Kufungua na kuimarisha Klabu za wapinga Rushwa 27.
Katika kuendeleza ushirikiano wa TAKUKURU na taasisi mbalimbali katika mapambano dhidi ya rushwa kikiwemo Chama cha Skauti Tanzania, kwa kushirikiana na Afisa Elimu Mkoa (ambaye ni Rais wa Skauti Mkoa) na Kamishna wa Skauti Mkoa, tuliweza kuwasilisha Kitabu cha “Mwongozo wa Mafunzo kwa Wawezeshaji wa kufundisha vijana wa Skauti kuhusu Kuzuia na Kupambana na Rushwa’’ kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ndiye Mlezi wa Skauti Mkoa. Mwongozo huu uliwasilishwa kwake kwa ajili ya kuelewa yaliyobainishwa kwenye kitabu hicho na kuweza kuendelea kushiriki katika kuhamasisha vijana na viongozi wa skauti kutumia mwongozo huo kuelimisha vijana wa Skauti katika juhudi za kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa katika Mkoa wetu.
Ushirikiano wa TAKUKURU na Chama cha Skauti Tanzania unatambulika kwa jina la TAKUSKA. Baada ya kukabidhi mwongozo huo kwa mlezi wa Skauti Mkoa, tumeendelea kutoa Elimu kwa Umma katika Shule za Sekondari zenye klabu za wapinga rushwa kwa kuwashirikisha wanafunzi ambao ni skauti pamoja na walezi wao katika shule husika pindi tunapo zitembelea kwa ajili ya kufungua na kuimarisha Klabu za wapinga Rushwa. Aidha, tunaendelea na mkakati wa utekelezaji wa Mwongozo huo kwa kushirikiana na viongozi wa skauti Mkoa, wilaya na katika shule zetu.
Lengo kuu la uelimishaji huu ni kuendelea kuhabarisha Umma juu ya madhara ya Rushwa katika jamii na Taifa kwa ujumla, sambamba na kuwaelimisha kuhusu vijana wa skauti kuhusu umuhimu wa kila mwananchi kushiriki katika Mapambano dhidi ya Rushwa na kwa kuzingatia Kauli mbiu ya “Kupambana na Rushwa ni Jukumu Langu” ili kila mwananchi awe na uelewa na ahamasike kushiriki katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Ndugu WanaHabari;
UZUIAJI RUSHWA
Katika utekelezaji wa jukumu la Uzuiaji Rushwa, TAKUKURU Mkoa wa Njombe, kwa kupitia Dawati la Uzuiaji Rushwa limekuwa likitekeleza jukumu hili kwa njia ya ufuatiliaji wa fedha za Umma kwa utaratibu wa PETS katika miradi ya maendeleo na uchambuzi wa mifumo.
- Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Katika kipindi hicho miradi mia moja na kumi na moja (111) yenye thamani ya shilingi 6,720,496,243.17 ilifanyiwa ufuatiliaji kwa lengo la kuzuia vitendo vya rushwa. Ufuatiliaji huo ulifanyika katika miradi ifuatayo:
Miradi kumi (10) ya Ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari kwa fedha za EP4R zilizotolewa mwezi Machi 2021. Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-
Mradi wa ujenzi wa madarasa mawili (2) wenye thamani ya sh. 40,000,000 na mradi wa ujenzi wa matundu kumi na mbili (12) ya vyoo yenye thamani ya sh. 13,200,000 katika Shule ya msingi Image.
- Mradi wa ujenzi wa madarasa mawili (2) wenye thamani ya sh. 40,000,000 na mradi wa ujenzi wa maabara moja (1) wenye thamani ya sh. 30,000,000 katika Shule ya Sekondari Kidegembye.
- Mradi wa ujenzi wa matundu kumi na mbili (12) ya vyoo katika Shule ya Msingi Lunguya wenye thamani ya sh. 13,200,000.
- Mradi wa ujenzi wa maabara tatu (3) (ya Chemistry, Physics na Biology) wenye thamani ya sh. 90,000,000, katika Shule ya Sekondari Kibena.
- Mradi wa ujenzi wa madarasa mawili (2) wenye thamani ya sh. 40,000,000 katika Shule ya Msingi Kibena.
- Mradi wa ujenzi wa matundu kumi na mbili (12) ya vyoo wenye thamani ya sh. 13,200,000 katika Shule ya Msingi Kibena.
- Mradi wa ujenzi wa matundu kumi na mbili (12) ya vyoo wenye thamani ya sh. 13,200,000 katika Shule ya Sekondari Maheve.
- Aidha,TAKUKURU mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Njombe, tumefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi tisini na sita (96) yenye thamani ya shilingi 5,110,000,000 kwa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 zilizotolewa mwezi Septemba 2021. Ufuatiliaji huo ulifanyika katika miradi ifuatayo:
JINA LA MRADI | THAMANI YA MRADI (Tshs.) |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya Sekondari Kibena | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matano shule ya Sekondari Maheve | 100,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matano shule ya Sekondari Mabatini | 100,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matano shule ya Sekondari Mpechi | 100,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Yakobi | 20,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Anne Makinda | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa manne shule ya Sekondari Kifanya | 80,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Uwemba | 20,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya Sekondari Uliwa | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Luhololo | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa manne shule ya Sekondari Matola | 80,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Mgola | 20,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Utalingolo | 20,000,000 |
Ujenzi wa Bweni katika shule ya Msingi Kibena | 80,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mulunga | 40,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya sekondari Lupembe | 20,000,000 |
Ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari Manyunyu | 80,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Ikuna | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mfriga | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Kidegembye | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Itipingi | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari J M Makweta | 40,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya sekondari Ninga | 20,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matano shule ya sekondari Sovi | 100,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya msingi kituo shikizi Itova | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Madeke S/M kituo shikizi Itembeli | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Shikizi Wangama | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili 2 shule ya msingi Shikizi Kihanga | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili 2 shule ya msingi Shikizi Maguvani | 40,000,000 |
Ujenzi wa Bweni moja kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Idofi | 80,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Shikizi Mfumbi | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Shikizi Muungano | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari Makambako | 80,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mlowa | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Deo sanga | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari Kitandililo | 80,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Maguvani | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Kipagamo | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Mahongole | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mukilima | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Mtimbwe | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Lyamkena | 60,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Mount Chafukwe | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Matamba | 40,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja shule ya Sekondari Kitulo | 20,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Isapulano | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Mwakavuta | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Iwawa | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Ipelele | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Ilumaki | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Lupalilo | 40,000,000 |
Ujenzi wa darasa moja Shule ya Sekondari Mang”oto | 20,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Lupila | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Ipepo | 40,000,000 |
Ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Ilungu | 40,000,000 |
Ujenzi wa jengo la huduma za dharura (EMU) | 300,000,000 |
Ujenzi nyumba za watumishi wa afya tatu kwa moja | 90,000,000 |
JUMLA | 5,110,000,000 |
- Pia tumefanya ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ifuatayo ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana.
- Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wanging’ombe katika kata ya Igwachanya wenye thamani ya sh.150, 000,000/=.
- Ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita moja (1KM) kuanzia Dombwela hadi Ikulu yenye thamani ya sh. 468,470,000/=.
- Ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita moja (1KM) kuanzia ukumbi wa kanisa la NLC hadi nyumba ya Luvanda yenye thamani ya sh. 500,000,000/=.
- Ujenzi wa vyumba viwili vya maabara wenye thamani ya sh. 60,000,000/= katika shule ya Sekondari Isapulano.
- Aidha tumefanya ufuatiliaji wa fedha za usimamizi wa chanjo ya UVIKO-19 kiasi cha sh.139, 226,243.17.
Lengo la ufuatiliaji wa miradi hii ni kuhakikisha kuwa thamani ya fedha (value for money) katika miradi ya maendeleo inafikiwa pamoja na kubaini uwepo wa vitendo vya rushwa au mianya ya rushwa ili kuweza kuchukua hatua za haraka kama vile kuchunguza, kutoa elimu kwa wananchi ambao ndio wanufaika wa miradi na pia kutoa ushauri kwa mamlaka husika kuhusu namna bora ya kuziba mianya ya rushwa iliyob ainika wakati wa ufuatiliaji.
Mapungufu machache yaliyobainika katika Ukaguzi wa miradi hiyo ambayo yangeweza kusababisha mianya ya rushwa, yameweza kufanyiwa kazi kwa kufanya vikao na wadau wa miradi husika pamoja na kutoa elimu kwa lengo la kuondoa mianya ya rushwa iliyopo na kuimarisha usimamizi wa miradi kwa kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni za manunuzi ya umma ili kupata miradi bora yenye kukidhi thamani ya fedha (Value for money) pamoja na kuanzisha uchunguzi.
Aidha, tunawaomba wananchi katika maeneo ambayo miradi mbali mbali inatekelezwa kuwa makini kuifuatilia kwani ushiriki wao ni silaha muhimu ya kufikia lengo la miradi hiyo. Tunawakumbusha wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kutimiza wajibu wao kwa weledi na uaminifu ikiwa ni pamoja na utunzaji mzuri wa nyaraka zinazohusiana na matumizi ya fedha za miradi husika zinazotolewa na Serikali au michango ya wananchi kwa urahisi wa rejea.
- Uchambuzi wa Mifumo
Ndugu WanaHabari;
Uimarishaji wa mifumo hufanyika kwa kufanya uchambuzi wa mifumo, kuweka mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa na kufanya utekelezaji wa mikakati hiyo.
Katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2021 TAKUKURU Mkoa wa Njombe tumefanya chambuzi za mifumo mitatu (03), Sambamba na warsha za kujadili matokeo ya chambuzi za mifumo hiyo na kuweka mikakati ya utekelezaji wa maazimio yaliyotokana na warsha zilizofanyika. Chambuzi hizo ni kama ifuatavyo:-
- Uchambuzi wa mfumo wa vihatarishi vya rushwa ya ngono katika sekta ya Elimu.
- Uchambuzi wa mfumo wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
- Uchambuzi wa mfumo wa uendeshaji wa shamba la maparachichi katika Halmashauri ya Mji Makambako lenye thamani ya sh. 23,089,925.
Lengo la uchambuzi wa mifumo hiyo ni kubaini uwepo wa vitendo vya rushwa au mianya ya rushwa ili kuweza kuchukua hatua za haraka kama vile kuchunguza, kutoa elimu kwa viongozi na wadau pia kutoa ushauri kwa mamlaka husika kuhusu namna bora ya kurekebisha mapungufu yaliyobainika ambayo yanatoa mianya ya rushwa.
Kupitia chambuzi hizi, baadhi ya mapungufu yanayopelekea mianya ya rushwa yalibainishwa na kwa kupitia warsha tulikaa na wadau husika kujadili matokeo ya chambuzi zetu na kuwekeana maazimio ya namna bora ya kuondokana na mianya hiyo ya rushwa.
Aidha, tunaendelea kuwakumbusha Wakurugenzi, Maafisa elimu, Viongozi wa vyama vya Walimu, Waratibu wa elimu, Wasimamizi wa ubora wa elimu na Walimu kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, katika kutukeleza majukumu yao na kujiepusha na vitendo vya rushwa ya ngono kwa weledi mkubwa na uadilifu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu. Pia taasisi za Serikali kuendelea kufanya manunuzi kwa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) na Wakala kutoa huduma bora zinazokidhi viwango.
Ndugu WanaHabari;
UCHUNGUZI
Katika kipindi husika, jumla ya taarifa 69 zilipokelewa. Mchanganuo wa taarifa hizo ni kama ifuatavyo; Sekta ya Afya 06, Mahakama 05, Polisi 03, TAMISEMI 25, Ujenzi (TANROADS) 02, Ardhi 05, Nishati (TANESCO) 01, Elimu 07, Fedha 05, TRA 02, Watu Binafsi 02, Utalii 01, Ofisi ya Mashtaka 01, Maji 01, Habari 01, Siasa 01 na Usafirishaji 01 ambapo taarifa zilizohusu rushwa zilikuwa 38 na uchunguzi wa awali umeanzishwa na unaendele. Taarifa zisizohusu rushwa zilikuwa 31, ambapo walalamikaji walielimishwa na kushauriwa ipasavyo baada ya kusikilizwa na pia kati ya hizo – taarifa mbili (2 ) zilihamishiwa Idara nyingine.
Aidha,katika kipindi husika, uchunguzi wa majalada 5 ya zamani ulikamilika na mashauri 2 yalifunguliwa mahakamani. Kwa sasa kuna jumla ya mashauri Matatu (03) yanayoendelea Mahakamani.
MIKAKATI TULIYOJIWEKEA KWA KIPINDI CHA JANUARI HADI MACHI, 2022
- Kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za vitendo vya rushwa na namna ya kushiriki katika Mapambano dhidi ya RUSHWA kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo. Utekelezaji huu utafanyika kwa njia mbalimbali zikiwemo kupitia mikutano ya hadhara (TAKUKURU INAYOTEMBEA), Kushiriki katika maonesho, Semina, kutoa mada kwenye taasisi, katika shule na kwa wanachama wa Klabu za wapinga Rushwa.
- Kuendelea kushirikiana na Viongozi wa skauti wilaya/shule katika uelimishaji wa vijana wa skauti namna ya kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mwongozo wetu wa Ushirikiano (TAKUSKA).
- Kuendelea kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa inatekelezwa kwa mujibu wa mikataba iliyofungwa au taratibu zinazokubalika ili kufikiwa kwa thamani ya fedha. Lengo kuu likiwa ni kuzuia vitendo vya hujuma na ubadhirifu wa fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya, kata au vijiji kwa maslahi ya watanzania.
- Kufanya chunguzi kwa wakati kwa taarifa zote za rushwa na ufisadi zitakazopokelewa kutoka kwa wananchi watakaofika katika ofisi zetu, zilizowasilishwa kwa njia ya barua au simu, zitakazo ibuliwa wakati wa utoaji wa Elimu kwa umma kwenye Mikutano ya hadhara pamoja na zitakazopatikana kutoka vyanzo vya SIRI.
- Kuwafikisha watuhumiwa Mahakamani baada ya kupata ushahidi wa kuthibitisha pasipo shaka, makosa ya rushwa au makosa mengineyo yatakayobainika kutendwa na wahusika au mhusika wakati wa uchunguzi wa makosa ya rushwa dhidi yake.
- Kuendeleza ushirikiano wenye kuleta tija katika utendaji wetu wa kazi na Idara au Taasisi nyingine mfano Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa, SKAUTI, Mahakama, Vyama vya Siasa na vyombo vingine vya dola,ska. Tunaamini kuwa kukosekana kwa ushirikiano madhubuti kati ya TAKUKURU na Idara au Taasisi nyingine, huleta changamoto katika Mapambano dhidi ya Rushwa – kwani mapambano dhidi ya rushwa ni jukumu la kila Mtanzania kwa maendeleo yake binafsi na kwa Taifa kwa ujumla. Daima tuitekeleze kauli mbiu hii ya : “ KUPAMBANA NA RUSHWA NI JUKUMU LANGU”
Ndugu Wana Habari;
Napenda kuwashukuru sana kwa namna mnavyotupatia ushirikiano katika kuuhabarisha Umma juu ya shughuli zinazotekelezwa na TAKUKURU Mkoa wa Njombe na kwa nchi nzima kwa weledi na ufanisi.
Ninawashukuru tena kwa ushirikiano mzuri na ninawatakia kazi njema na ushiriki mwema katika Mapambano Dhidi ya Rushwa.
Imetolewa na:
Kassim H.S Ephrem
Mkuu wa TAKUKURU (M) Njombe Nambari ya Simu: 0738 150 170