MARA, OKT – DES 2021

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

NDUGU WANAHABARI

Kwanza kabisa tunamshukuru Mwenyezi Mungu kutukutanisha kwa mara nyingine tena leo hii kwa ajili ya kuuhabarisha umma kuhusu kazi zilizotekelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mara. Taasisi hii imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2019. Jukumu mojawapo la TAKUKURU ni kuhamasisha ushiriki wa makundi mbalimbali katika kuzuia vitendo vya rushwa, na leo tunawapa taarifa ya TAKUKURU Mkoa wa Mara ya utekelezaji wa jukumu hilo na mengine kwa robo ya Oktoba hadi Disemba, 2021.

NDUGU WANAHABARI

Kwanza, tunatambua kwamba maadili ni mwenendo mwema na pia linamaanisha misingi, taratibu na kanuni zilizokubalika kwenye jamii kuwa mwongozo wa mahusiano au matendo mema na ni nguzo muhimu katika usimamiaji wa haki. Pamoja na shughuli nyingi zilizofanyika katika robo hii tumeshiriki katika siku ya Maadili kitaifa kwa kutoa mafunzo kwa wananchi mbalimbali na kwa kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji maalumu. Tulitoa vyakula na vifaa mbali mbali kwa Wazee na Watoto yatima katika Kituo cha kuwalea cha Makoko Musoma Mjini.

NDUGU WANAHABARI

Kwa kipindi tajwa tulitembelea klabu za wapinga rushwa na kuhamasisha uhai wake ambapo jumla ya klabu 42 zimeimarishwa. Kazi zingine za uelimishaji zilizofanyika ni Semina 24 na Mikutano ya Hadhara 28 ambapo kero mbalimbali za wananchi zinazohusiana na rushwa zilisikilizwa na kutafutiwa ufumbuzi.

TAKUKURU INAYOTEMBEA ilifika katika Kata ya Etaro, kijiji cha Rukuba ambacho ni Kisiwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kwa kushirikiana na watumishi wa Idara ya Afya kusikiliza na kutatua kero za wananchi kuhusu upatikanaji wa dawa na uadilifu wa watumishi wa Zahanati ya kijiji hiki.

Pia katika Wilaya ya Serengeti kwa kushirikiana na watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii tulitembelea Kikundi cha Yesu ni Jibu katika Kata ya Uwanja wa Ndege na kusikiliza kero zao ambazo majibu yake yalipatikana hapo hapo.

USHIRIKIANO NA CHAMA CHA SKAUTI – TAKUSKA:

Katika kipindi husika, TAKUKURU Mkoa wa Mara iliweza kuutambulisha Mwongozo wa Mafunzo kwa Wawezeshaji wa Kufundisha Vijana wa Skauti Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa. Mwongozo huu tayari umetambulishwa hadi ngazi za Wilaya tayari kwa kuanza kutumika – lengo likiwa ni kuwajenga vijana katika misingi ya Uzalendo, Uwajibikaji na Kutojihusisha na Vitendo vya Rushwa.

NDUGU WANAHABARI

Pili, Mbinu nyingine inayotumiwa na TAKUKURU kuzuia vitendo vya rushwa ni ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na utambuzi wa mianya ya rushwa unaolenga katika kutoa ushauri wa namna ya kuiziba.

Katika robo iliyoisha, TAKUKURU Mkoa wa Mara ilijikita katika ufuatiliaji wa matumizi ya fedha ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 yote ikiwa na thamani ya shs. 9,780,000,000/=

TAKUKURU Mkoa wa Mara, kwa kushirikiana na Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Watumishi toka Ofisi za Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zote za Mkoa wa Mara, imefuatilia utekelezaji wa miradi hiyo tangu hatua za awali ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana.

Yaliyobainika katika ufuatiliaji huu ni kwa baadhi ya Wilaya, kazi za ujenzi wa madarasa kuchelewa kuanza, kutokana na uhaba wa vifaa vya ujenzi kama simenti na mabati kutokana na uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.

Vilevile, mvua kubwa iliyonyesha katika baadhi ya maeneo iliharibu  miundombinu ya barabara na kusababisha kuongezeka kwa gharama za usafirishaji wa vifaa vya ujenzi katika maeneo ya ujenzi.

Mapungufu mengine ni kwamba baadhi ya mafundi walioomba kazi kujitoa katika hatua za mwisho za kusaini mkataba kwa kisingizio kuwa fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika ni kidogo. Hata hivyo baada ya magereza kuombwa kuifanya kazi hiyo na mafundi kutoka Wilaya nyingine, wakandarasi wa awali walikubali kuikamilisha kazi hiyo.

Kasoro nyingine ni baadhi ya majengo kujengwa chini ya kiwango na kuelekezwa kuvunjwa na kujengwa upya ili yaweze kukidhi viwango na usalama wa wanafunzi na walimu. Mfano Tarime DC, majengo katika Sekondari ya Gibaso, madarasa mawili yalivunjwa na Sekondari ya Kitawaso madarasa matatu yalivunjwa na kujengwa upya  kwa maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na timu yake.

Tunawaomba wananchi katika maeneo ambayo miradi hii inatekelezwa kuwa makini kuifuatilia kwani ushiriki wao ni silaha muhimu ya kufikia lengo la miradi hiyo. Aidha, tunawakumbusha wakandarasi na wasimamizi hiyo kutimiza wajibu wao kwa weledi na uaminifu.

Pia tumekagua miradi mingine 11 kwenye sekta za elimu, afya na barabara. Lengo ni kuhakikisha kwamba fedha za umma zinazoelekezwa kwenye miradi hiyo zinatumika kwa ufanisi na uaminifu. Ufuatiliaji huu umewezesha marekebisho mbali mbali kufanyika katika hatua za awali na hivyo kufanikisha miradi hii kuwa bora.

Aidha, zimefanyika chambuzi 10 za mifumo ya utendaji katika usimamizi wa mitihani katika Vyuo vya Kati kikiwemo Chuo Cha Uuguzi Tarime na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare. Pia zilifanyika Warsha 2 za kujadili matokeo ya chambuzi za mifumo kwa kuwashirikisha wadau. Katika chambuzi hizo hakuna viashiria vya rushwa vilivyobainika.

NDUGU WANAHABARI

Tatu, Katika kipindi husika, jumla ya taarifa 142 zilipokelewa ambapo taarifa za rushwa zilikuwa 98 na taarifa 44 hazikuhusu rushwaTaarifa 44 ambazo hazikuhusu rushwa, watoa taarifa walielimishwa na kushauriwa na kisha taarifa hizo kuhamishiwa Idara nyingine. Aidha, katika taarifa 98 zinazohusu rushwa, taarifa 87 uchunguzi wake unaendelea na taarifa 11 uchunguzi umefungwa kwa kukosa ushahidi.

Mchanganuo wa taarifa 142 kisekta ni kama ifuatavyo:

NA.