KINONDONI, OKT – DES 2021

TAKUKURU MKOA WA KINONDONI YASHINDA KESI MBILI (2) MAHAKAMANI

Ndugu wana habari;

Ni wakati wetu mwingine tena, ambapo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, tunahabarisha umma kuhusu utendaji kazi wetu kwa kipindi cha miezi mitatu kupitia kwenu kama ulivyo utaratibu wetu wa kawaida. Mnakaribishwa sana katika mkutano huu kwa ajili ya kufanya kazi hii muhimu sana kwetu na kwa wananchi wote kwa ujumla. 

Katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba, 2021, TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni imeendelea na majukumu yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kulingana na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka  2007 na imefanikiwa kutekeleza mpango kazi wake katika Idara zote ambazo ni Uchunguzi, Uzuiaji Rushwa na Elimu kwa Umma.

Ndugu Wanahabari,

Uchunguzi:

Katika kipindi hicho, TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni imepokea jumla ya taarifa mia mbili ishirini na tisa (229). Kati ya taarifa hizo, taarifazinazohusiana na vitendo vya Rushwa zilikuwa Mia moja Thelathini na Tatu (133) na zisizohusu masuala ya Rushwa ni Tisini na Sita (96).

Katika taarifa hizo 133 zilizohusu rushwa, tumefungua majalada ya uchunguzi ambapo majalada yaliyofunguliwa na kufikia hatua ya uchunguzi wa kina ni manne (4) na majalada manne (4) yamekamilika na kwenda Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Majalada 125 yaliyobaki, uchunguzi wake bado unaendelea.

Mchanganuo wa kisekta wa malalamiko 229 yaliyopokelewa ni kama ifuatavyo: Asasi Binafsi taarifa 99, TAMISEMI taarifa 36, Mahakama 13, Polisi 9, Elimu 9 na nyingine nyingi ambazo zimelalamikiwa kwa idadi ndogo.

Katika kipindi husika, kesi mpya moja (1) imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni na kufanya jumla ya kesi zinazoendelea mahakamani kuwa kesi Kumi na moja (11). Kesi mbili (2) zimetolewa hukumu na Jamhuri imeshinda kesi zote.

Kwa upande wa taarifa 96 ambazo hazikuhusu rushwa, taarifa 65 watoa taarifa wake wameshauriwa hatua za kuchukua ili kupata haki zao na taarifa 33 zimehamishiwa idara nyingine kwa hatua zaidi.

Ndugu wanahabari;

Uelimishaji Umma:

TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni iliendelea na jukumu la kuelimisha umma kupitia njia mbalimbali, lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya rushwa.

Uelimishaji ulifanyika kwa kuendesha semina kumi na moja (11) kwa makundi mbalimbali na mikutano ya hadhara mitano (5). Pia tumeshiriki katika onesho Moja (1) na kuimarisha klabu za wapinga rushwa ishirini na tatu (23), kipindi cha redio kimoja (1) na kufanya mkutano na waandishi wa habari mara moja (1).

Vilevile TAKUKURU Kinondoni kwa ushirikiano na ofisi za Ilala na Temeke, ilishiriki katika utambulisho wa Mwongozo wa Mafunzo kwa Wawezeshaji wa Kufundisha Vijana wa Skauti kuhusu Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwongozo huo wa mafunzo unatokana na mkakati uliopo kati ya TAKUKURU na Chama cha Skauti Tanzania ambao ulizinduliwa rasmi Machi, 2020. Mkakati huu wa TAKUKURU na Skauti (TAKUSKA), ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu ambao lengo lake ni kuwaongoza wawezeshaji ili wawafundishe vijana wa Skauti kuwa waadilifu, wawajibikaji na wazalendo kuanzia ngazi yake binafsi, katika familia, shuleni, jamii na Taifa.

Ndugu Wanahabari,

Katika kufanikisha mpango wa TAKUKURU INAYOTEMBEA, kipindi hiki tulishirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuelimisha wananchi katika wiki ya huduma iliyojulikana kwa jina la “ONE STOP JAWABU”.

Uelimishaji huo ambao ulifanyika kwa siku saba (7) kuanzia tarehe 16/12/2021 hadi 22/12/2021 katika eneo la Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama Dar es salaam, ulilenga kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya ya Kinondoni kwa urahisi na kwa gharama nafuu katika eneo moja.

TAKUKURU pia ilielimisha jumla ya Taasisi arobaini (40) zilizoshiriki katika maonesho hayo. Baadhi ni; CRDB, NIDA, RITA, UHAMIAJI, NMB, DAWASCO, TRA, OSHA, TARURA, EWURA, TTCL, BRELA, CHF, NSSF, TLS Afisa Kazi na Idara zote za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Uelimishaji uliofanyika umewawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na kwa kutumia muda mfupi kiasi cha kuomba zoezi hilo lifanyike tena kwa wakati mwingine.

Ndugu wanahabari;

Uzuiaji Rushwa:

Katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2021, ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni ilifanya ufuatiliaji wa fedha za miradi sh 2,992,808,667.6 ambapo sh 72,808,667.6 ni za uhamasishaji wa chanjoya Uviko 19 na sh 2,920,000,000 za ujenzi wa madarasa. Lengo la ufuatiliaji wa miradi ni kuhakikisha kuwa fedha zinatumika kwa usahihi kama ilivyoelekezwa kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na muda husika.

Katika kipindi husika, TAKUKURU mkoa wa Kinondoni imefuatilia miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari katika Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO 19 na jumla ya Shule za Sekondari ishirini na tano (25) zenye vyumba vya madarasa 146 vilifuatiliwa.Ufuatiliaji huu haukubaini mapungufu yoyote na tayariujenzi wa shule hizo umekamilika na wanafunzi wameshaanza masomo.

Pia TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni ilifanya chambuzi za mifumo  mbili (02)  ambazo ni  Uchambuzi wa tathmini ya utendaji kazi wa Wakala wa Ununuzi wa Umma Serikalini (GPSA) lengo likiwa ni  kufanya tathmini ya wakala wa hud