TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI
TAKUKURU YAFUATILIA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 16.5
NDUGU WANAHABARI
Kwanza kabisa tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha leo hii kwa ajili ya kuuhabarisha umma wa Watanzania, kuhusu utendaji kazi zilizotekelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita katika kipindi cha miezi mitatu, kuanzia Oktoba hadi Desemba, 2021. Taarifa hii inajumuisha utendaji kazi wa ofisi ya Mkoa na zile za wilaya za Chato, Bukombe, Mbogwe na Nyang’hwale, ambapo kazi mbalimbali zimetekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2019 kwa lengo la kuhamasisha na kukuza utawala bora na kupambana na rushwa.
Kazi hizi zimetekelezwa kupitia njia ya Uzuiaji wa vitendo vya rushwa kwa kufanya udhiti na uelimishaji umma pamoja na kupambana na wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na makosa yahusianayo kwa kufanya chunguzi zinazopelekea kufungua mashtaka mahakamani.
NDUGU WANAHABARI
Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2021 TAKUKURU Mkoa wa Geita imetekeleza kazi zifuatazo:
- Uzuiaji wa vitendo vya Rushwa:
TAKUKURU Mkoa wa Geita imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na udhibiti, ambapo jumla ya Miradi ya Maendeleo thelathini na tatu (33) yenye thamani ya Shilingi 16,598,305,391.23 (Bilioni kumi na sita, miatano tisini na nane milioni, laki tatu na tano elfu mia tatu tisini na moja na senti ishirini na tatu) ilifuatiliwa. Kati ya miradi hiyo, miradi ishirini na mbili (22) ilikuwa ni miradi iliyotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO 19. Miradi hii ni ya Sekta za Afya, Elimu, Maji na Ujenzi, na ilifuatiliwa kwa lengo la kujiridhisha iwapo kuna thamani halisi ya fedha zilizotumika na kujiridhisha iwapo kuna ufujaji; ucheleweshaji wa makusudi wa mradi; uchepuzi wa rasilimali za mradi pamoja na namna jamii inavyoshirikishwa katika utekelezaji wa miradi hiyo. Miradi iliyofuatiliwa ni kama ifuatavyo:
Wilaya ya Geita.
- Ufuatiliaji wa Fedha za kutekeleza shughuli mbalimbali za Utoaji Chanjo ya Uviko 19 katika halmashauri ya wilaya ya Geita wenye thamani ya shilingi 31,412,788.47.
- Miradi ya Ujenzi wa Madarasa 347 Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kwa gharama ya shilingi 6,940,000,000/=.
- Miradi ya Ujenzi wa Madarasa 61 Katika Halmashauri ya Mji wa Geita kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kwa Gharama ya shilingi 1,220,000,000/=
Wilaya ya Chato.
- Ujenzi wa Kituo cha Afya Mapinduzi Buseresere wenye thamani ya shilingi 777,000,000/=uliohusisha ujenzi wajengo la OPD, theatre, maternity pamoja na nyumba ya mtumishi.
- Ujenzi wa barabara ya TARURA kutoka Ilemela hadi Kachwamba yanye urefu wa km 8.5 ya thamani ya sh. 970,300,000/=
- Ujenzi wa madarasa ya programu ya TCRP (Tanzania Covid Recovery Programme), ikihusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 151 katika Shule za Sekondari 27 zenye thamani ya shilingi 3,020,000,000/=.
- Ujenzi wa vyumba vya madarasa 32 ya shule za msingi (Shikizi) 10 yenye thamani ya shilingi 640,000,000/=.
Wilaya ya Bukombe.
- Uchimbaji wa visima vinne (4) vya maji katika vijiji vya Namonge na Katome, vyenye thamani ya shilingi 107,285,600/=.
- Ujenzi wa Barabara 2 za Uyovu-Namonge-Namalandula na barabara ya Namonge – Ilyamchele zenye thamani ya shilingi 413,887,900/=
Wilaya ya Nyanghwale.
- Ufuatiliaji wa Fedha za kutekeleza shughuli mbalimbali za Utoaji Chanjo ya Uviko 19 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wenye thamani ya shilingi 19,095,595/=.
- Ujenzi wa Kituo cha Afya NYIJUNDU katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wenye thamani ya shilingi 250,000,000/=.
- Ufuatiliaji wa fedha za ujenzi wa vyumba 54 vya Madarasa kwa shule 12 za Sekondari na Shule za Msingi Shikizi 4 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale vyenye thamani ya shilingi 1,080,000,000/=. Ujenzi huo unatekelezwa kwa fedha za UVIKO 19.
Wilaya ya Mbogwe.
- Ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu wilayani Mbogwe katika Shule ya Msingi Masumbwe lenye thamani ya shilingi 80,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 9 Shule ya Sekondari Nyakasaluma wenye thamani ya shilingi 180,000,000/=,
- Ujenzi wa madarasa 3 katika Shule ya Sekondari Iponya wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 3 Shule ya Sekondari Lugunga wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 8 Shule ya Sekondari Nyasato wenye thamani ya shilingi 160,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 4 Shule ya Sekondari Mbogwe wenye thamani ya shilingi 80,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 3 Shule ya Sekondari Isangijo wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 3 Shule ya Msingi Kadoke wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 4 shule ya sekondari Ngemo wenye thamani ya shilingi 80,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 3 shule ya Sekondari Nanda wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 4 Shule ya Sekondari Ilolangulu wenye thamani ya shilingi 80,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 3 Shule ya Sekondari Ikobe wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa madarasa 2 Shule ya Msingi Kagongo wenye thamani ya
shilingi 40,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 6 Shule ya Sekondari Isebya wenye thamani ya shilingi 120,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 3 Shule ya Sekondari Ikunguigazi wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 3 Shule ya Sekondari Nhomolwa wenye thamani ya shilingi 60,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 6 Shule ya Sekondari Lulembela wenye thamani ya shilingi 120,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 11 Shule ya Sekondari Masumbwe wenye thamani ya shilingi 220,000,000/=.
- Ujenzi wa Madarasa 2 katika kituo shikizi cha Ilyamchele wenye thamani ya shilingi 40,000,000/=.
- Mradi wa matumizi ya fedha za utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 wenye thamani ya Tshs. 18,734,302.89/=.
- Ujenzi wa mradi wa maji wa Nanda (Nanda water supply project) wenye thamani ya shilingi 340,889,205/=.
Mapungufu machache yaliyobainika katika ufuatiliaji wa miradi hiyo ambayo yangeweza kusababisha uwepo wa mianya ya rushwa yamefanyiwa kazi kwa kufanya vikao na wadau wa utekelezaji wa miradi husika pamoja na kutoa elimu kwa lengo la kuondoa mianya hiyo. Hii ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi kwa kusisitiza uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Manunuzi ya Umma ili kupata miradi bora yenye kukidhi thamani ya fedha (Value for money.
Vilevile, katika kipindi husika, tumefanya chambuzi nane (8) za mifumo ya utoaji wa huduma katika Sekta za Elimu, Kilimo, Afya na Mapato, ambapo mianya ya rushwa iliyobainishwa, ilijadiliwa kupitia warsha 4 zilizofanyika kati ya TAKUKURU na wadau kujadili matokeo ya chambuzi zetu na kuwekeana maazimio ya namna bora ya kuondokana na mianya hiyo ya rushwa.
NDUGU WANAHABARI
Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2021 Elimu ya mapambano dhidi ya rushwa imetolewa katika makundi mbalimbali ili kuhamasisha umma kushiriki mapambano dhidi ya Rushwa. Mbinu mbalimbali za kuelimisha zimetumika kwa kufanya Semina 37; Mikutano ya Hadhara 41; Uimarishaji wa Klabu za Wapinga Rushwa 41 katika Shule za Msingi na Sekondari; Utoaji wa taarifa kwa vyombo vya habari 6; Maonesho 5; Uandishi wa makala au habari 3; vipindi vya redio 3; Mkutano na waandishi wa habari 1; na kugawa kwa wananchi, machapisho mbalimbali yenye ujumbe wa kukemea vitendo vya rushwa.
Pia katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2021 tumeendelea kutatua kero za wananchi zinazohusiana na vitendo vya Rushwa, kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuendelea na mpango wa kuwashirikisha vijana wa Skauti Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa katika misingi ya Uadilifu, Uwajibikaji na Uzalendo kupitia mkakati wa pamoja wa TAKUKURU NA SKAUTI (TAKUSKA). Vilevile, tumeendelea kuwaelimisha watumishi wa Sekta za Umma na Binafsi kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kujiepusha na ubadhirifu, wizi na matumizi mabaya ya ofisi za umma.
NDUGU WANAHABARI
Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2021 tumeendelea kupokea taarifa za malalamiko. Katika kipindi husika, tumepokea taarifa 95 za malalamiko ambapo taarifa zilizohusu rushwa zilikuwa ni 68 na 27 zilikuwahazihusiani na rushwa. Taarifa 27 ambazo hazikuhusu rushwa, wahusika walipatiwa ushauri na kuelekezwa mahali sahihi pa kuwasilisha malalamiko yao.
Taarifa hizo 95 zilizopokelewa zilihusu sekta zifuatazo:
Serikali za Mitaa malalamiko 36, Madini 7, Elimu 7, Afya 6, Kazi 6, Polisi 6, Ardhi 5, Sekta Binafsi 4, Fedha 4, Ujenzi 2, Nishati 2, Maliasili 2, Mahakama 1, Mifuko ya jamii 1, Uhamiaji 1, Biashara 1, Jeshi la akiba 1, Manunuzi 1, Michezo 1 na Vyama vya ushirika 1
Uchunguzi wa awali wa malalamiko 68 yanayohusu rushwa umeendelea kufanyika ambapo:
- Taarifa 51 bado zipo katika uchunguzi wa awali
- Taarifa 6 zimefunguliwa majalada ya uchunguzi
- Taarifa 2 zimefungwa,
- Taarifa 2 zimehamishiwa ofisi nyingine
- Majalada 7 uchunguzi wake umekamilika
Aidha kesi zilizofunguliwa mahakamani katika kipindi hiki ni 5 na kufanya jumla ya kesi zilizoendeshwa mahakamani kufikia 18. Katika kipindi husika kesi 1 ilitolewa maamuzi na Jamhuri ilishinda.
NDUGU WANAHABARI Kazi zote hizi zimeweza kutekelezwa ikiwa ni mafanikio ya ushirikiano tunaoupata kutoka kwa wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya rushwa, mkiwemo ninyi waandishi wa habari.
NDUGU WANAHABARI
Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, 2021 ofisi iliendelea na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi kwa kuwatembelea na kusikiliza changamoto zao kwa utaratibu wa TAKUKURU INAYOTEMBEA na kuzipatia majibu ambapo katika kipindi hicho mikutano tisa (09) ilifanyika katika maeneo mbalimbali.
Katika mikutano hiyo wananchi waliuliza maswali na kupewa ufafanuzi juu ya maswali mbalimbali waliyouliza, walipewa elimu juu ya dhana ya rushwa, namna ya kutoa taarifa na kuelezwa dhumuni la kuwafikia mahali walipo ikiwa ni pamoja na kuwapa nafasi ya kusikilizwa ili kujua changamoto za rushwa zinazowakabili kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi. Aidha kero mbalimbali zilipokelewa na kuwasilishwa kwa idara husika za Serikali ili kupatiwa ufumbuzi.
NDUGU WANAHABARI
MKAKATI WA JANUARI HADI MACHI, 2022
Katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2022 tumejipanga kujikita katika UZUIAJI RUSHWA hususan kwa kuendelea kutatua kero za wananchi zinazohusiana na vitendo vya Rushwa pamoja na kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi. Vilevile tutaendelea na mpango wa kuwashirikisha vijana wa Skauti Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwaelimisha katika misingi ya Uadilifu, Uwajibikaji na Uzalendo kupitia mkakati wa pamoja wa TAKUKURU NA SKAUTI (TAKUSKA). Pia tumejipanga kuendelea kuwaelimisha watumishi wa Sekta za Umma na Binafsi ili wawe waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kujiepusha na ubadhirifu, wizi na matumizi mabaya ya ofisi za umma.
Pia, katika kuhakikisha kuwa tunawafikia wananchi wengi zaidi wa mkoa wa Geita, TAKUKURU Mkoa wa Geita imetenga siku moja kila mwezi ambapo itakuwa inawafuata wananchi walipo kupitia utaratibu wa TAKUKURU INAYOTEMBEA, ili kusikiliza na kutatua kero zao dhidi ya rushwa. Vilevile, tutaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa ile ya kimkakati pamoja na ya Sekta za Afya na Elimu. Aidha, tutafuatilia utekelezaji wa maazimio tuliyokubaliana na wadau katika warsha za kujadili mianya ya rushwa iliyobainishwa katika chambuzi mbalimbali tulizokwisha zifanya.
NDUGU WANAHABARI
Wito wetu kwa wananchi wa mkoa wa Geita ni kwamba waendelee kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa kwa vitendo na wasibaki watazamaji.
Tunawaasa wana Geita, wajihadhari na watu wanaojifanya kuwa ni Maafisa wa TAKUKURU na wasisite kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika ofisi za TAKUKURU kwa kupiga simu ya bure 113, *113# au kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 113 au kupitia TAKUKURU APP.
Vilevile, tunawaasa watumishi wa Sekta za Umma na Binafsi mkoani Geita, wawe waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kujiepusha na ubadhirifu, wizi na matumizi mabaya ya ofisi za umma ili kuwaondolea kero ya rushwa wananchi wetu, pindi wanapohitaji huduma kutoka kwao.
Ahsanteni kwa kunisikiliza. Sote tuseme “KUPAMBANA NA RUSHWA NI JUKUMU LANGU”
IMETOLEWA NA:
Azza E. Mtaita,
Naibu Mkuu wa TAKUKURU (M) Geita,
Simu: 0738 150079