Lengo Kuu ni kuelimisha vijana wa Skauti ili waichukie rushwa na kushiriki kuzuia na kupambana nayo wakingali wadogo.
Mkakati huu utawezesha wawezeshaji kuwa na uelewa wa pamoja wa maudhui ya elimu na kuongeza ufahamu wa masuala kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na itachangia kuwafanya wanafunzi shuleni na vyuoni kuwa wazalendo, waadilifu na wawajibikaji zaidi katika jamii na Taifa kwa ujumla. Aidha, tunaamini kuwa, Mwongozo huu utawanufaisha pia walimu, wanafunzi na wadau wengine watakaousoma kwa madhumuni ya kujifunza kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.