Utafiti ni mbinu mojawapo inayotumika kupata taarifa zinazowesha uimarishaji mifumo zinazofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuzuia rushwa. Kazi hii hufanyika kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 7(a) na (c) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 na sheria nyingine za nchi. Aidha, utafiti unaweza kufanywa na watu au taasisi nyingine kwa kuratibiwa na TAKUKURU, mfano ‘baseline surveys’ na ‘service delivery surveys’.