Mwongozo wa kufundishia vijana wanachama wa Skauti kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa, utaanza kutumika rasmi hivi karibuni nchi nzima. Mwongozo huu umetokana na makubaliano ya Mkakati wa Ushirikiano kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Chama Cha Skauti Tanzania (CST), wa kushirikisha vijana wa Skauti katika mapambano dhidi ya rushwa.