Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na mambo mengine, ina jukumu la kuzuia rushwa kupitia uimarishaji mifumo. Katika kufikia lengo hili, TAKUKURU hufanya
- utafiti
- uchambuzi wa mifumo
- ufuatiliaji wa matumizi wa rasilimali za umma (PETS)
- kuwakutanisha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya kutekeleza mapendekezo ya TAKUKURU ya kudhibiti rushwa
- kufuatilia utekelezaji wa mikakati hiyo