TAKUKURU imekuwa ikiwatumia wadau mbali mbali katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa mapambano yanategemea juhudi za wadau mbali mbali. Moja ya wadau ambao wanatumiwa na TAKUKURU ni wanafunzi kupitia klabu za wapinga rushwa. Mnamo mwezi Mei, 2007 TAKUKURU ilianzisha kampeni ya kufungua klabu za wapinga rushwa katika shule za sekondari Tanzania Bara ambapo Mkurugenzi Mkuu Dkt. Edward Hoseah alizindua klabu ya wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Makongo ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kampeni hii. Zoezi hili liliendelea hata katika vyuo vya elimu ya juu na shule za msingi. Lengo la kuanzisha klabu hizi ni kuwajenga wanafunzi kimaadili kwa kuwafanya watambue madhara ya rushwa ili waichukie katika maisha yao na kuchukua hatua za kuzuia na kupambana nayo hatimaye kujenga jamii ya watu waadilifu.
Miongoni mwa kazi zinazofanywa na klabu ni
- kuwaelimisha wafunzi wenzao kuhusu rushwa na madhara yake
- kutoa taarifa za vitendo vya rushwa TAKUKURU
- kutoa elimu ya rushwa kwa njia ya maigizo, uandishi wa makala, insha, uchoraji wa katuni, midahalo, kuimba nyimbo, kushiriki katika matamasha yanayoandaliwa na TAKUKURU, kushiriki katika shughuli za kijamii kama kutembelea wagonjwa, wazee ama wahitaji mbali mbali, kupanda miti na mengineyo