Vigogo MSD kizimbani kwa rushwa

 

Washtakiwa walikana shtaka na upande wa Mashtaka uliieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi umekamilika na kuiomba mahakama  ipange tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali na kwamba haukuwa na pingamizi la dhamana kwa washtakiwa.

Wakili wa utetezi Gerald Nangi aliiomba mahakama iwapatie wateja wake dhamana yenye masharti nafuu. Hakimu Mwijage aliwataka washtakiwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka serikalini,Taasisi au Mashirika binafsi yaliyosajiliwa ambao wangesaini bondi ya Tsh. 20,000,000/=. Aidha, kila mshtakiwa alitakiwa kutoa hati ya mali isiyohamishika yenye thamani isiyopungua Tsh.200, 000,000/=.

Washtakiwa  wote walitimiza masharti ya dhamana na wako nje kwa dhamana. Kesi imeahirishwa hadi tarehe Machi 21, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Februari15, mwaka jana Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alitangaza kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne wa MSD akiwemo Cosmas Mwaifwani kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Tsh.bilioni1.5 ili kupisha uchunguzi. Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na  Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Fedha; Misanga Muja, Mkurugenzi wa Ugavi; na Henry Mchunga, Mkurugenzi wa Manunuzi.Taarifa ya kuwasimamisha kazi ilitolewa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akikabaidhi vitanda kutoka MSD kwa ajili ya wodi ya wazazi.