Waziri Angellah Kairuki afungua mkutano wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa Afrika Mashariki

Baadhi ya wajumbe wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki (EAAACA) uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha 29 – 30 Novemba, 2016.
Wanafunzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Arusha wakigani ngojera kuhusu ushirikishwaji wa vijana na jamii nzima katika mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki (EAAACA) uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha 29 – 30 Novemba, 2016.
Wakurugenzi Wakuu wa Shirikisho la Mamlaka za Kuzui na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki (EAAACA) wakiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na baadhi ya wajumbe mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 10 wa EAAACA uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha 29 – 30 Novemba, 2016.
Wajumbe na Wakuu wa Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Shirikisho la Mamlaka  za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki (EAAACA) uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha 29 – 30 Novemba, 2016.