MHIFADHI BARABARA MSAIDIZI TANROADS AHUKUMIWA KWENDA JELA KWA MAKOSA YA RUSHWA

Na Stella Mafuru

Mahakama ya Wilaya ya  Kinondoni imemhukumu Shaban Mahamudu Kyomile (34), Mhifadhi barabara Msaidizi Tanroads, kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh. 500,000/= baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya rushwa.

Hukumu hii ilitolewa na hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mhe. Bi.Carolina Kiliwa Alhamisi iliyopita baada ya upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakimkabili mshtakiwa bila kuacha shaka.

Awali Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Bi. Stella Mafuru aliieleza Mahakama kuwa tarehe 16/12/2015 mshtakiwa alipokea Sh.200, 000/= toka kwa Shafii Abdi Shaban, mfanyabiashara wa Azam Ice Cream, ili aweze kumpatia baiskeli zake mbili alizokuwa amezishikilia kwa kosa la kufanya biashara katika eneo la hifadhi ya barabara ya Tanroads katika kituo cha daladala cha Mbezi Luis.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani tarehe 22 Desemba,2015 kwa mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Mshtakiwa  alikuwa akijitetea mahakamani mwenyewe na aliachiwa huru baada ya kulipa faini ya shilingi 500,000/=.

Vigogo MSD kizimbani kwa rushwa

Na Mussa Misalaba

Vigogo wawili wa Bohari ya Dawa (MSD) wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakikabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya madaraka.

Vigogo hao ni Cosmas Mwaifwani, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MSD na Fredrick Rubanga ambaye alikuwa  kaimu Meneja wa Manunuzi wa MSD.Washtakiwa walifikishwa mahakamani na Jamhuri mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mheshimiwa Respicius Mwijage. Upande wa Jamhuri uliongozwa na waendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Leonard Swai na Aneth Mwavika.

Waendesha Mashtaka waliiambia mahakama kuwa kati ya tarehe 1Machi,2013 na 19Machi,2013 katika ofisi za Makao Makuu ya MSD Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa MSD, walitumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa na kusaini  mabadiliko ya mkataba uliopelekea Kampuni ya H.H Hillal kupata manufaa yasiyo halali ya Tsh.482,266,000/=.

Read more ...

Makala ya Mdahalo wa Maadili

Download Here

Waziri wa Sheria na Katiba azindua wiki ya Huduma kwa wananchi

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu Wiki ya Huduma kwa Wananchi wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Viwanja vyaMnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2016.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wananchi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2016.

Read more ...

Waziri Angellah Kairuki afungua mkutano wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa Afrika Mashariki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki (EAAACA) uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha 29 – 30 Novemba, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino L. Mlowola akitoa maelezo kwa wajumbe wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Shirikisho la Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki (EAAACA) uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha 29 – 30 Novemba, 2016.

Read more ...

Subcategories