Tue10132015

Wajue Wahalifu wa makosa ya rushwa

Click here to see list of shame

Search

Back You are here: Home Home Investigation Prosecution Wakurugenzi BoT mahakamani kwa uhujumu uchumi

Home

Wakurugenzi BoT mahakamani kwa uhujumu uchumi

Wafanyakazi wa BoT wakiwa Mahakamani
Wafanyakazi wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Septemba 15, 2009 walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasara kubwa ya zaidi ya shilingi bilioni mia moja na nne.

Washtakiwa hao ni Bw. Simon Jengo, Bw. Kisima Mkango, Bw. Bosco Kimela na Bw. Ally Bakari ambao katika kesi hiyo Na. 09/2009 wanakabiliwa na mashtaka matatu.

Akisoma mashtaka dhidi yao, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Ben Lincolin alisema katika shtaka la kwanza dhidi ya Jengo na Mkango, mwaka 2004, Jengo akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki na Mkango akiwa Naibu Mkurugenzi wa Fedha wa BoT, wakifahamu na kwa madhumuni ya kumdanganya mwajiri wao, walitumia bei ya uchapishaji wa noti za mkataba mkuu wa 2001 katika mkataba wa nyongeza wa mwaka 2004 na kuuwasilisha Sehemu ya Sheria ya Benki hiyo kwa mapitio.

Katika shtaka la pili linalomkabili Jengo peke yake, ilielezwa kuwa katika tarehe tofauti mwaka 2005, aliagiza kuchapishwa kwa kiasi kikubwa cha noti  za fedha kupitia mkataba wa nyongeza wa mwaka  2005 ikilinganishwa na ule ulioandaliwa na Idara husika ya BoT.

Matukio hayo mawili, kwa mujibu wa mashtaka, yalikuwa kinyume na Kifungu cha 6 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa Sura ya 329 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 ikisomwa pamoja na aya ya 1 ya Jedwali la Kwanza na Vifungu 57 (1) na 60 vyote vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu Uliopangwa Sura 200 (iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002).

Shtaka la nne linawakabili washtakiwa wote wakiwemo Kimela (aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria) na Bakari (Mkurugezni wa Huduma za Kibenki), ambapo ilielezwa kuwa kati ya mwaka 2004 na 2007, waliandaa mkataba wa nyongeza ulioonyesha bei kubwa ya uchapishaji wa noti za fedha ikilinganishwa na bei halisi ya mkataba mkuu wa mwaka 2001. Hatua hiyo, kwa mujibu wa aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza na Vifungu 57 (1) na 60 vyote vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu Uliopangwa Sura 200 (iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002), iliisababishia Serikali hasara ya shilingi 104, 158, 536, 146.

Baada ya mashtaka hayo kusomwa, wakili wa utetezi waliitaka Mahakama kuitupa kesi hiyo kwa sababu Kifungu cha 65 cha Sheria ya Benki Kuu kinatoa kinga dhidi ya mashtaka kwa wateja wao kwa utekelezaji wowote wa majukumu yao uliofanywa kwa ‘nia njema’. Wakili Mpare Mpoki alisema wateja wao wanashtakiwa kinyume cha kifungu hicho na kwamba Mahakama ilikosea kuipokea kesi hiyo. Aliendelea kudai kuwa mashtaka hayo yangekuwa na nguvu iwapo yangeeleza kuwa washtakiwa walitekeleza majukumu yao kwa ‘nia mbaya’.

Akijibu hoja za upande wa utetezi, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU alieleza Mahakama kuwa kwa mujibu wa mashtaka, washtakiwa kwa ufahamu wao walifanya vitendo hivyo kwa makusudi ya kumdanganya mwajiri wao na hivyo hoja ya ‘nia njema’ haina msingi. Kwa sababu hiyo aliitaka Mahakama itupilie mbali ombi la upande wa utetezi na kuendelea na taratibu za kimahakama.

Bw. Lincolin aliongeza kuwa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu Uliopangwa Sura 200 (iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002), kinaelekeza kuwa kesi za uhujumu uchumi zifunguliwe kupitia Mahakama ya Wilaya na hivyo Mahakama hiyo ilikuwa na mamlaka ya kupokea kesi hiyo.

Awali, kabla ya upande wa mashtaka kusoma mashtaka, mawakili hao wa utetezi waliitaka Mahakama hiyo isipokee kesi hiyo kwa madai kuwa wateja wao wana kinga dhidi ya mashtaka. Mawakili hao, Bw. Mpoki na Bw. Mabere Marando walisema Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kupokea kesi hiyo kwa sababu upande wa mashtaka ulikosea kuwafungulia mashtaka watuhumiwa.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Samwel Maweda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alitupilia mbali ombi hilo la upande wa utetezi  kwa maelezo kuwa ni lazima taratibu za Mahakama zifuatwe kwanza kwa kesi kupokelewa ndipo mawakili hao watapata nafasi ya kutoa utetezi.

Matukio katika picha

Sample image Sample image
Sample image Sample image
Sample image mcc
                                                         

       

 

                                                     
 

Visitors Counter

260397
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
851
1021
4154
248776
15371
34212
260397

Your IP: 54.221.27.136
Server Time: 2015-10-13 14:26:31