BW. EKWABI WEBSTER TEKERE MUJUNGU – MKURUGENZI WA IDARA YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU TAKUKURU ACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UMOJA WA AFRIKA YA USHAURI KUHUSU MASUALA YA RUSHWA (AU ADVISORY BOARD ON CORRUPTION).

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

BW. EKWABI WEBSTER TEKERE MUJUNGU – MKURUGENZI WA IDARA YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU TAKUKURU ACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UMOJA WA AFRIKA YA USHAURI KUHUSU MASUALA YA RUSHWA (AU ADVISORY BOARD ON CORRUPTION).

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu – TAKUKURU Bw. Ekwabi Mujungu, amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri juu ya Masuala ya Rushwa – ‘African Union Advisory Board on Corruption’.

Uchaguzi huo ulifanyika katika kikao cha 24 cha Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kilichofanyika Januari, 2015 - Addis Ababa Ethiopia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 11/02/2015 na ofisi ya Makao Makuu ya umoja huo iliyoko ADDIS ABABA ETHIOPIA, wadhifa huo utadumu kwa muda wa miaka miwili.

Bodi hii ambayo makao makuu yake yapo jijini Arusha – Tanzania, jukumu lake kuu ni kushauri na kusimamia masuala ya Rushwa kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Wajumbe wengine waliochaguliwa katika Bodi hii ni kutoka nchi za Cote d’lvoire, Togo, Burundi, Ghana, Benin, Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Kenya na Zimbabwe.

Tanzania inajivunia kuwa Mjumbe wa Bodi hii tangu kuanzishwa kwake ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hoseah alikuwa Mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi hii kwa kipindi cha 2011-2014.

 

Imetolewa na Doreen J. Kapwani - Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Jumanne tarehe 17/02/2015

Mkurugenzi TAKUKURU aapishwa kuwa mjumbe AU

mujungu

BW. EKWABI WEBSTER TEKERE MUJUNGU – MKURUGENZI WA IDARA YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU TAKUKURU AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UMOJA WA AFRIKA YA USHAURI KUHUSU MASUALA YA RUSHWA (AU ADVISORY BOARD ON CORRUPTION).

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu – TAKUKURU Bw. Ekwabi Mujungu, ameapishwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri juu ya Masuala ya Rushwa – ‘African Union Advisory Board on Corruption’.

Uapisho huo ulifanyika Jumatatu tarehe 04/05/2015 katika kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe 35 kutoka nchi wanachama pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Jiji la Arusha.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kilifanya uchaguzi wa viongozi wake ambapo Ghana alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Zimbabwe alichaguliwa kuwa Katibu na Kenya walichaguliwa kuwa Rapouteur.

Bodi hii ambayo Makao Makuu yake yapo jijini Arusha – Tanzania, jukumu lake kuu ni kushauri na kusimamia masuala ya Rushwa kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Wajumbe wengine waliochaguliwa katika Bodi hii ni kutoka nchi za Cote d’lvoire, Togo, Burundi, Ghana, Benin, Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Kenya na Zimbabwe.

Tanzania inajivunia kuwa Mjumbe wa Bodi hii tangu kuanzishwa kwake ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hoseah alikuwa Mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi hii kwa kipindi cha 2011-2014.

 

Imetolewa na Doreen J. Kapwani - Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Jumatano tarehe 13/05/2015

Dkt. Hoseah achaguliwa tena kuwa Mjumbe wa AU-ABC

 Director General of PCCB at his office

 

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt. Edward Hoseah amechaguliwa tena kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Nchi za Umoja wa Afrika (African Union Advisory Board on Corruption) kuanzia Januari 2013. Uchaguzi huu umefanyika katika Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama, uliofanyika Januari 28, 2013 Mjini Addis Ababa – Ethiopia.