JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AKABIDHI TAARIFA YA AWALI YA UCHUNGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KWA WAZIRI HASUNGA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Brig. John Mbungo (Kushoto), leo Aprili 16, 2020 amekabidhi TAARIFA YA AWALI YA UCHUNGUZI KUHUSU VYAMA VYA USHIRIKA kwa Mhe. Japhet Hasunga (Kulia) ambaye ni Waziri wa Kilimo. Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dodoma katika ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo.

 AWALI: Novemba 26, 2019, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga alimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Ruhwa nchini – TAKUKURU Brig Jen John Mbungo, TAARIFA YA MUHTASARI WA UCHAMBUZI WA UKAGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019.

 Taarifa hii ilihusu ukaguzi uliofanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (Co-operative Audit and Supervision Corporation – COASCO) ambapo TAKUKURU ilitakiwa kuchunguza uwepo wa vitendo vya ubadhirifu na rushwa katika matumizi ya fedha za ushirika nchini Tanzania.

 Kupitia uchunguzi huu ambao unafanyika kwa awamu, TAKUKURU tayari imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Bilioni 8.8 (Shilingi Bilioni 8,898,661,156.88).