KILA MMOJA ANA UWEZO WA KUSHIRIKI KATIKA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA.

media

Novemba 9 mwaka 2015 kuna picha ya video ilisambaa katika mitandao ya kijamiii kuhusu Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye aliomba na kupokea rushwa wilayani Handeni mkoa wa Tanga.

Uovu kama huu unatokea katika maeneo mengi kila siku lakini wananchi hawakuwa na ujaziri wa kurekodi na kuwasilisha Polisi au TAKUKURU video za aina hii ambazo ushahidi wake uko wazi.

TAKUKURU inatoa pongezi nyingi kwa ujasiri na mfano mzuri uliooneshwa na mwananchi huyu ambaye ameweza kushiriki kikamilifu katika kutimiza wajibu wake wa kuzuia na kupambana na Rushwa nchini.

Aliyekuwa askari katika Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Anthony Temu (46) mwenye namba F. 785 wa Kituo cha Polisi Kabuku wilayani Handeni alifukuzwa kazi siku mbili tu baada tukio hilo kuripotiwa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji, kufukuzwa kazi kwa askari huyo kumetokana na taarifa ya kuomba na kupokea rushwa iliyopatikana kupitia mitandao ya kijamii.

Kamanda Mwombeji alieleza pia kuwa mtuhumiwa huyo ameshakabidhiwa kwa maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tanga pamoja na kielelezo ambacho ni video iliyokuwa ikirushwa kwenye mitandao ya kijamii ili waendelee kumshughulikia kwa upande wa jinai katika makosa ya kuomba na kupokea rushwa.

TAKUKURU tunatoa wito kwa kila Mtanzania kushirikiana nasi katika jitihada hizi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwani athari zake zinamgusa kila mmoja wetu.

 

Prosecution

SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA BOT, TRA, TANESCO, REA NA ARDHI WAPANDISHWA KIZIMBANI 11 Sep 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania – TAKUKURU, imewafikisha katika mahakama...

More detail
MAWAZIRI WAWILI WA ZAMANI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA TISA 10 Sep 2015

  Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa...

More detail
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Songea anaswa kwa Rushwa 10 Sep 2015

Mnamo tarehe 03/03/2015 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Mwanasheria wa Halmashauri...

More detail