Aliyekuwa Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha ahukumiwa kwenda jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemhukumu kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya TSh.1.5000,000/= aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Johanes Monyo, baada ya kumkuta na hatia ya kosa la kutumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa ajira kwa Chacha Wambura kinyume na sheria za utumishi wa Umma.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama tarehe 15/11/2016 mbele ya Hakimu Mfawidhi Mheshimiwa Agustino Rwezile katika shtaka la Jinai namba 18/2015 lililokuwa linaendeshwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Violet Machary, Monica Kijazi na Hamidu Simbano.

Mshtakiwa alikutwa na hatia na mahakama katika kosa la kutangaza na kuajiri nafasi ya Afisa Raslimali Watu bila ya kuwa na kibali cha Idara ya Utumishi kinyume na Kifungu cha 29(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8/2007 kitendo kilichopelekea Chacha Wambura kujipatia manufaa ya ajira na mshahara asiostahili.

Mshtakiwa alilipa faini ya TSh.1, 500,000/= na kujinasua kwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela katika gereza la Kisongo, Arusha.

 

Prosecution

SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA BOT, TRA, TANESCO, REA NA ARDHI WAPANDISHWA KIZIMBANI 11 Sep 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania – TAKUKURU, imewafikisha katika mahakama...

More detail
MAWAZIRI WAWILI WA ZAMANI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA TISA 10 Sep 2015

  Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa...

More detail
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Songea anaswa kwa Rushwa 10 Sep 2015

Mnamo tarehe 03/03/2015 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Mwanasheria wa Halmashauri...

More detail