Maofisa wawili wa TFF Mahakamani kwa rushwa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam, maofisa wawili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Martin Chacha Mecky na Juma Matandika, kujibu shtaka la kushawishi hongo ya Tsh.25, 000,000/=.

Martin Mecky ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano na Juma Matandika ambaye ni Msaidizi wa Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania, wanadaiwa kushawishi kiasi hicho cha hongo toka kwa viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Geita (GRFA) na Timu ya Mpira wa Miguu Geita (GGSC) ili wazitumie kuwashawishi viongozi wa TFF na Idara ya Uhamiaji Tanzania ili watoe maamuzi ya kuishusha daraja Timu ya Polisi Tabora na kuipandisha daraja daraja la kwanza la Ligu Kuu Tanzania timu ya GGSC.

Washtakiwa walifikishwa mbele ya Mh. Huruma Shaidi, Hakimu Mkuu Mkazi na walikana shtaka la jinai namba 403/2016 lililosomwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Leonard Swai na Odesa Horombe. Waendesha mashtaka waliiambia mahakama kwamba washtakiwa walitenda kosa tarehe 4 Februari, 2016 kwenye ofisi za TFF Makao Makuu, Dar es Salaam, ambalo ni kinyume na kifungu cha 15(a)(1) na (2) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa uchunguzi wa shauri umekamilika na uko tayari kwa usikilizwaji wa hoja za awali katika tarehe ambayo ingepangwa na mahakama. Hakimu Shaidi alikubali ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hadi tarehe 30 Novemba, 2016. Washtakiwa walipewa dhamana na mahakama baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao walisaini dhamana ya Tsh.5, 000,000/=.

 

Prosecution

SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA BOT, TRA, TANESCO, REA NA ARDHI WAPANDISHWA KIZIMBANI 11 Sep 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania – TAKUKURU, imewafikisha katika mahakama...

More detail
MAWAZIRI WAWILI WA ZAMANI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA TISA 10 Sep 2015

  Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa...

More detail
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Songea anaswa kwa Rushwa 10 Sep 2015

Mnamo tarehe 03/03/2015 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa Mwanasheria wa Halmashauri...

More detail