TAKUKURU imepongezwa na gazeti la Habari leo kutokana na kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio na kwa kuzingatia maagizo ya Rais John Pombe Magufuli katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 unaomalizika.

Kupitia toleo lake Namba 03774 la Aprili 20, 2017 ukurasa wa 6 gazeti la Habari Leo limeipongeza TAKUKURU kwa kuokoa zaidi ya bilioni 12.3 ambapo Sh. milioni 912 ni za mishahara hewa, Sh.bilioni 8.3 zilitokana na ukwepaji wa ushuru kupitia mfumo wa kielektroniki wa EFD, Sh.bilioni 2.6 kutokana na ubadhirifu na kiasi kingine cha Sh.milioni 794.18 kiliokolewa katika maeneo mengine.

Aidha, gazeti hili limeipongeza TAKUKURU kwa kufanya vizuri katika uendeshaji wa kesi mahakamani, kuwezesha kutaifishwa kwa mali za washtakiwa wa rushwa, na udhibiti wa mianya ya rushwa katika mifumo ya hati za kusafiria na sheria na kanuni za uanzishwaji na usimamizi wa maduka ya dawa muhimu za binadamu.

“Hizi ni fedha nyingi ambazo zitasaidia serikali katika baadhi ya maeneo muhimu.Tunaamini kupatikana kwa fedha hizo kunaongeza hali pia kwa taasisi nyingine kuiga mfano”,limeandika gazeti.

Tunalipongeza gazeti hili kwa kuona na kuthamini mchango wa TAKUKURU katika kukabiliana na uharifu nchini katika kipindi hiki ambacho serikali inapambana kudhibiti mapato yake yanayoishia mfukoni mwa watu wasiowaaminifu na tunaamini pongezi hizi ni chachu kwetu kuweza kufanya vizuri zaidi kwa mwaka wa fedha ujao. Fingua Kiambatisho