Viongozi wakuu wa Kamati ya Utendaji ya AACAA waliochaguliwa ni Emmanuel Ollita Ondongo wa Jamhuri ya Congo ( Rais), El Hadji Mansour Tall wa Senegal (Makamu wa Kwanza wa Rais), Phiri Kapetwa wa Zambia (Makamu wa pili wa Rais), CP Isdorre Ndihokubwayo wa Burundi (Katibu Mkuu).

Tanzania iliwakilishwa vizuri na Daniel Pundu, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Udhibiti, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na aliwasilisha  mada iliyohusu “Ubunifu na mambo mapya katika mapambano dhidi ya rushwa: Uzoefu wa Tanzania”.

Mbali na uchaguzi wa viongozi wa Kamati ya Utendaji ya AACAA, Mkutano Mkuu ulijadili mambo mbalimbali ambayo nchi wanachama wa mamlaka za kupambana na rushwa Afrika zipatazo 38 zinaweza kuyaboresha katika mapambano dhidi ya rushwa.

Umoja wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika (Africa Anti – corruption Authorities Association – AACAA) ambao awali ulifahamika kama   Umoja wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika (Association of Anti- Corruption Authorities in Africa – AAACA) ulianzishwa Juni 21, 2011 Bujumbura, Burundi.

Kati ya malengo ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mamlaka za Kumpambana na Rushwa Afrika (AACAA) ni pamoja na kuwezesha utekekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Umoja wa Afrika  na Mkataba wa Kuzuia Rushwa wa Umoja wa Mataifa.

Mkataba wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Umoja wa Afrika pamoja Mkataba wa Kuzuia Rushwa wa Umoja wa Mataifa unazitaka nchi wanachama kushirikiana na kusaidiana katika misaada ya kisheria, usimamizi wa sheria, uchunguzi wa pamoja, ufuatiliaji na kurejesha mali zilizopatikana kwa rushwa, kubadilishana uzoefu, na ushirikiano wa kiufundi.

  kuimarisha na kusaidia ushirikiano baina ya nchi wanachama katika kuzuia, kubaini, kuchunguza, kukusanya na kutoa ushahidi wa uendeshaji wa kesi mahakamani na uendeshaji wa kesi za rushwa na makosa yanayofanana nayo.

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa unaichukulia  rushwa  kuwa moja wapo ya  vikwazo vikubwa vya maendeleo kwa kuwa huharibu mfumo wa uchumi, huharibu utawala wa sheria, hukimbiza wawekezaji, huzuia upataji wa huduma zitolewazo na nchi, na huharibu misingi ya democrasia

Mamlaka za kupambana na rushwa zina umuhimu mkubwa  pia katika utekelezaji wa lengo namba 16 la Agenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya umoja wa Mataifa (Sustainable Development Goals – SDGs) iliyopitishwa tarehe 25 Septemba, 2015 katika Mkutano Maalum  wa Umoja wa Mataifa wa wakuu wan chi  na Serikali.

Mkutano Mkuu ujao wa AACAA umepangwa kufanyika Aprili 2018 nchini Senegal na wajumbe waliafikiana kuwa iwapo kutatokea nafasi ya uongozi ikawa wazi, nafasi hiyo itajazwa na mtu ambaye atateuliwa na Mamlaka ambayo mhusika alitokea.