Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, CP. Diwani Athumani ameahidi kuongoza jukumu la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa nchini kwa kuzingatia maelekezo aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Dira, Dhima na Misingi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.